Home » Mhitimu Wa ”First Class Honours” Ajiua Baada Ya Kushindwa Kupata Kazi

Mhitimu Wa ”First Class Honours” Ajiua Baada Ya Kushindwa Kupata Kazi

Michael Kibet/photo courtesy

Familia moja ya Nandi iko katika majonzi kufuatia kifo cha jamaa yao ambaye inasemekana alijitoa uhai baada ya kukosa kupata kazi.

 

Michael Kibet alihitimu na shahada ya kwanza “first class honour “katika kozi ya mawasiliano na teknolojia ICT kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jomo Kenyatta mnamo 2021.

 

Kijana huyo wa miaka 26 alikuwa na matumaini ya kupata kazi lakini baada ya miaka miwili, juhudi zake za kupata kazi hazikuzaa matunda.
Inasemekana alijitoa uhai katika boma la kakake huko Lessos baada ya kutafuta nafasi za ajira bila mafanikio.

 

Chifu wa eneo hilo David Rugut aMEthibitisha kisa hicho, akisema marehemu alijinyonga nje ya nyumba ya kakake kutokana na kufadhaika.
Alisema familia hiyo haikupoteza tu mwanafunzi mahiri bali mtaalamu anayetegemewa katika eneo lote la Chepsangor.

 

“Kwa kweli tumehuzunishwa na kumpoteza Michael. Alikuwa kijana mchapakazi na mwenye nidhamu katika eneo letu. Alimaliza maisha yake kutokana na kuchanganyikiwa kulingana na kaka yake.”

 

Hadi kifo chake, Kibet alikuwa akiishi na mamake nesi mstaafu na mama asiye na mume, ambaye amekuwa akiwasomesha watoto wake peke yake baada ya kifo cha mumewe.

 

Mwili wa marehemu ulihamishwa hadi kwenye Mazishi ya Samaritan huko Kapsabet huku maandalizi ya mazishi yakiendelea. Atazikwa Ijumaa, Juni 9, 2023.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!