Azimio Watoa Sababu Ya Kutohudhuria Mkutano Wa Maombi Ya Kitaifa
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga na washirika wake Martha Karua, Kalonzo Musyoka na Eugene Wamalwa wamekosa kuhudhuria maombi ya Kitaifa Jumatano katika Hoteli ya Safari Park jijini Nairobi.
Hii ni siku moja baada ya viongozi wa muungano wa Azimio La Umoja One Kenya kutangaza kutohudhuria hafla hiyo na kuipuuza na kusema kuwa ni “kufuru” kwa Mungu.
Azimio hata hivyo iliwapa wabunge uhuru wa kuchagua kuhudhuria au kutohudhuria maombi hayo.
Miongoni mwa wabunge wa Azimio waliohudhuria ni Mwakilishi wa Wanawake wa Nairobi Esther Passaris, ambaye aliwaambia waandishi wa habari kuwa angetamani Odinga ahudhurie lakini anaheshimu uamuzi wake wa kutohudhuria, ambao alihusisha na kutoheshimiwa na serikali ya Kenya Kwanza.
Maombi ya kitaifa yapaswa kuhubiri amani na utangamano, huku yakiwaleta viongozi kutoka pande zote za kisiasa pamoja.
Mchanganuzi wa masuala ya kisiasa Daktari Abdul Noor anatoa kauli hii akisisitiza ni wakati viongozi wawache unafiki wa kuomba ilhali mioyo yao inalenga kinyume.
Akizungumza mapema leo, Noor alisema wakenya sasa wanatarajia kuona matunda kutoka kwa viongozi waliowachagua