Home » Majambazi Wamfunga Mlinzi Kabla Ya Kuiba Kanisani

Waumini wa kanisa la PCEA huko Molo kaunti ya Nakuru wameamkia habari za kushangaza hii leo Jumanne Asubuhi baada ya wezi kuvamia kanisa na kuiba mali ya thamani isiyojulikana.

 

Kulingana na viongozi wa kanisa hilo, walipokea simu za kuhuzunisha kutoka kwa majirani baada ya afisa wa Usalama wa Kanisa kupatikana akiwa amefungwa kamba kwenye uwanja wa kanisa hilo.

 

Aidha Inaaminika kuwa majambazi hao waliingia kanisani kupitia dirishani, huku maafisa wakidai walikuwa wakilenga pesa zilizokusanywa Jumapili wakati wa hafla ya Chama cha Wanawake ambapo pesa hizo zilihamishiwa kwenye akaunti ya kanisa.

 

Miongoni mwa vitu vingine vilivyoibwa ni Piano, amplifier, vitabu vya nyimbo na vitu vingine.

 

Waumini wa kanisa hilo wamelaani kitendo hicho cha ukosefu wa usalama huku wakiwataka polisi wa Molo kufanya doria mara kwa mara usiku na mchana ili kukabiliana na ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama.

 

Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI huko Molo walifika katika eneo la uhalifu wakianzisha uchunguzi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!