Home » Okiya Omtatah Afika Kortini
While speaking on NTV, Omtatah said the legislator, who he did not reveal, handed Ksh. 10,000 to him to aid in photocopying of his petition papers.

Okiya Omtatah Photo courtesy

Seneta wa Busia Okiya Omtatah ameelekea katika Mahakama Kuu kupinga masharti ya Mswada wa Fedha wa 2023.

 

Katika wasilisho lake, Omtatah ameteta kuwa Mswada huo ulikuwa kinyume na katiba na hivyo kuomba mahakama kuingilia kati.

 

Miongoni mwa masuala hayo, Omtatah ameangazia katika ombi lake ni makato ya lazima ya mishahara ili kuunga mkono ajenda ya Rais William Ruto ya Makazi ya bei nafuu, ambapo Wakenya hawawezi kulazimishwa.

 

Omtatah amedokeza kuwa Seneti na Bunge la Kitaifa zilifaa kujadili Mswada huo kabla ya kuwasilishwa.

 

Ombi lake linakuja siku chache baada ya Ruto kumsihi Omtatah kutopinga Mswada wa Fedha wa 2023 mahakamani.

 

Aidha wakenya wamekuwa wakiwarai bunge wao kutopitisha mswaada huo huku wabunge wakiwa katika hali ya kuchanganyikiwa ikiwa wataupitisha ama la wengine wakihisi kuwadanya wapiga kura nao wengine wakihisi watakaidi agizo la rais.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!