Home » Wauguzi Wanne Washtakiwa Kwa Kuvuna Viungo Vya Mwili

Picha kwa hisani

Afisa wa mkoa wa Tabora Magharibi nchini Tanzania amesema Wauguzi wanne katika mkoa huo watafikishwa mahakamani kwa kosa la kuvuna viungo vya watoto mapacha.

Kamati iliyoundwa kuchunguza tukio hilo iligundua kuwa miili ya mapacha hao waliozaliwa kabla ya wakati wao ilikuwa imeharibika baada ya kufariki.

 

Mama ya mapacha hao alikuta macho ya watoto wake yametobolewa na sehemu ya ngozi yao ikiwa imetoka kwenye paji la uso.

 

Mkuu wa mkoa wa Tabora, Batilda Buriani alisema wauguzi hao ambao wanashikiliwa na maafisa wa polisi ambapo pia wamesimamishwa kazi.

 

Alisema uvunaji wa viungo hivyo unahusishwa na uchawi.

 

Wauguzi hao waliipotosha kamati ya uchunguzi kwa madai ya uwongo kwamba miili hiyo ilihifadhiwa katika wadi ya wazazi wakati, ilipatikana katika chumba cha wauguzi, Bi Buriani aliongeza.

 

Ripoti hiyo pia inaeleza kuwa pacha hao walifariki dunia kutokana na ukosefu wa huduma za watoto wachanga, ambazo hazikupatikana katika kituo walichozaliwa.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!