Home » Seneta Osotsi: Uteuzi Wa Kenya Kwanza Ndio Mwanzo Wa Ufisadi

Seneta Osotsi: Uteuzi Wa Kenya Kwanza Ndio Mwanzo Wa Ufisadi

Seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi amedai kuwa uteuzi uliofanywa na serikali ya Kenya Kwanza unachochea ufisadi.

 

Katika mahojiano na runinga moja hii leo Jumatatu, Seneta huyo ametoa maoni kuwa baadhi ya watu wanaodaiwa kuhusika katika sakata ya sukari wanafanya kazi kwa karibu na rais.

 

Seneta huyo ameendelea kudai kuwa uteuzi unaofanywa na serikali haulengi kuwasilisha masuala ya kimsingi yanayohusu wananchi bali wale walioteuliwa kuchuma mapato.

 

Katika kueleza jinsi maafisa wanavyojipanga kupata pesa kupitia ufisadi, ametoa mfano wa wajumbe wa bodi ya usambaji vifaa vya matibabu KEMSA ambao kulingana naye wanastahili kupata takriban Ksh.320,000 kwa mwaka lakini wakaishia kupata zaidi.

 

Seneta huyo amemtaka rais kuangalia ustahimilivu wa wafanyikazi anaowateua serikalini.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!