Home » Umma Waalikwa Kuutazama Mwili Wa Mukami Kimathi

Serikali imealika umma kuutazama mwili wa Mukami Kimathi mkewe shujaa Dedan Kimathi Jumamosi, Mei 13, katika makafani ya Lee jijini Nairobi.

 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Dkt Raymond Omollo, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi iliyotwikwa jukumu la kuandaa mazishi hayo, amesema shughuli hiyo itafanyika kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa moja asubuhi.

 

Mazishi yatafanyika siku iyo hiyo nyumbani kwake Njabini, Kaunti ya Nyandarua.

 

Mukami alifariki Jumamosi iliyopita, Mei 5, alipokuwa akipokea matibabu katika Hospitali ya Nairobi. Alikuwa na umri wa miaka 96.

 

Kulingana na bintiye Nyawira Kimathi, mkongwe huyo alilazwa hospitalini baada ya kupata matatizo ya kupumua.

 

Mukami alikuwa miongoni mwa wapigania uhuru wa Mau Mau waliozuiliwa katika Gereza la Kimathi Maximum wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Kenya.

 

Mke wa marehemu Dedan Kimathi atakumbukwa kwa kusukuma Serikali kutafuta mwili wa mumewe ambao umezikwa kwenye kaburi lisilojulikana katika Gereza la Kamiti Maximum.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!