Zari Amtambulisha Mchumba Mpya Kwa Mama Yake

Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda, Tanzania pamoja na Afrika ya Kusini, Zarina Hassan amemfikisha mpenzi wake Shakib Lutaaya katika kaburi la mama yake mzazi.
SOMA PIA:ZARI: Men Cheat For Stupid Things Like Brown Thighs, Babygirl; Cheat For Money
Zari alilifanya hilo wakati alipofika nchini Uganda na ikawa vyema kwa yeye kumfikisha mpenzi wake huyo katika kaburi la mama yake kwa ajili ya utambulisho huo siku ya Alhamisi.
Katika maudhurio hayo ya kuhiji kaburi la Halima Hassan likiwa ndilo jina la mama huyo, Zari aliambatana pia na baba yake mzazi, mpenzi wake pamoja na wanafamilia wengine ambao waliwasindikiza katika eneo hilo.
Mama mzazi wa Zari Halima Hassan alifariki mwaka 2017 wiki kadhaa tu baada ya kumpoteza aliyekuwa mume wake Ivan ambaye pia ni baba wa watoto wake watatu.
Kwa sasa, Zari yuko amezama penzini na kijana huyo wa miaka 31 na miaka ya hapo nyuma Zari alifanikiwa kupata watoto wengine wawili na mwanamuziki kutokea nchini Tanzania Nassib Abdul ambaye pia anajulikana kwa jina la kikazi Diamond Platnumz