Home » Waziri Machogu Ahamisha Mwalimu Mkuu Wa Mukumu Girl Na Kuvunja Bodi

Waziri Machogu Ahamisha Mwalimu Mkuu Wa Mukumu Girl Na Kuvunja Bodi

CS Machogu Orders Students Be taught For 6 Hours On Weekdays

Education CS Ezekiel Machogu Image:File

Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu amefanya mabadiliko kadhaa katika Shule ya Upili ya Mukumu Girls katika Kaunti ya Kakamega.

 

Machogu aliyetembelea taasisi hiyo, amemhamisha mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Frida Ndolo na kubainisha kuwa Serikali inaendelea na uchunguzi wa tukio lililosababisha vifo vya wanafunzi watatu na mwalimu mmoja.

 

Nafasi ya Mkuu wa Shule imechukuliwa na Jane Mmbone, ambaye atahudumu katika wadhifa huo kwa siku zijazo.

 

Hapo awali Mmbone aliwahi kuwa Mkuu wa Shule ya Upili ya Shikoti, pia katika Kaunti ya Kakamega.

 

Waziri Machago pia ametupilia mbali bodi ya Usimamizi wa shule hiyo na kuahidi kuteua wajumbe wapya.

 

Uamuzi wa Machogu wa kumhamisha Mwalimu Mkuu Fridah Ndolo umetiliwa shaka mara moja na baadhi ya Wakenya waliohisi kama mamlaka kama hayo yalikuwa hifadhi ya Tume ya Huduma ya Walimu nchini TSC.

 

Aidha Sheria ya Tume ya Utumishi wa Walimu ya 2012 inatoa mamlaka ya kuajiri, kuhamisha au kumfukuza mwalimu, na si wala si Waziri.
Hata hivyo, waziri wa Elimu anaruhusiwa na Sheria kutangaza uhamisho wa walimu pekee.

 

Uhamisho wa Fridah pia ulijadiliwa wakati wa mkutano na Gavana wa Kaunti ya Kakamega Fernandes Baraza wakati wa ziara ya Machogu.

 

Machogu leo amefanua ziara hiyo kwa Gavana Barasa na Mkuu wa Mkoa wa Magharibi Samson Irungu ambapo amefanya mkutano mfupi kuhusu mkurupuko wa ugonjwa katika kaunti hiyo.

 

Jana ijumaa, Wizara ya Afya ilibaini kuwa ugonjwa huo uliosababisha vifo vya wanafunzi watatu na mwalimu katika Shule ya Upili ya Wasichana ya Mukumu katika Kaunti ya Kakamega ulisababishwa na unywaji wa maji machafu.

 

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Afya Patrick Amoth alisema kuwa matokeo ya vipimo yalionyesha athari za bakteria –inayofahamika kama… Ente-rotoxigenic E. coli na Salmonella typhi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!