Home » Wanaohitaji Ufafanuzi Kuhusu Tuzo Za TMA Wakaribishwa BASATA

Tuzo za TMA

 

Baada ya tuzo za Tanzania Music Awards kuleta mtetemo kwa wasanii, mratibu wa tuzo hizo Bwana Mrisho  mtumwa ameendelea kutoa ufafanuzi juu ya vipengele vilivyopo katika tuzo hizo.

 

SOMA PIA:Wafahamu Washindani Wa Tuzo Za Music Awards

 

Akizungumza na kituo cha redio cha TBC, mratibu huyo amezidi kutolea ufafanuzi juu ya uteuzi wa vipengele katika tuzo hizo za TMA ya kuwa ni jopo ndilo linalofanya maamuzi baada ya wasanii kukusanya kazi zao na kuwa kujiona bora ni kudharau kazi ya mwingine. Bwana Mrisho amesema ya kuwa ….

 

 

Asitokee mtu akasema EP au album yake ni bora kuliko ya mtu mwingine, hiyo ni kudharau kazi ya mtu mwingine”.

 

 

Katika sakata hilo la tuzo pia Mratibu huyo alieleza ya kuwa wapo wasanii waliolalamika ya kuwa hawakupeleka kazi zao hivyo menejimenti zao kuhusika na hatua zote mpaka kufika kwa kazi hizo na siyo BASATA kwamba walifanya hatua zozote.

 

 

Sambamba na hilo pia Mbosso alikaribishwa katika ofisi za BASATA endapo atakuwa na changamoto au kuhitaji ufafanuzi kutokana na malalamiko yake juu ya EP yake ya Khan kutokuwepo katika kipengele cha Albumu bora.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!