Home » KRG Azungumza Baada ya Akothee Kukosa Kumualika Kwenye Harusi

KRG Azungumza Baada ya Akothee Kukosa Kumualika Kwenye Harusi

Rapa kutoka nchini Kenya KRG the Don ameonyesha hisia zake baada ya mwanamuziki wa Kenya Akothee kushindwa kumualika kwenye harusi yake na mchumba wake Mzungu Omosh iliyofanyika jana katika hoteli ya Windsor.

 

Katika video iliyosambazwa kwenye Instagram, KRG alimtaja Akothee kwa kufanya sherehe ya kifahari na kukosa kumwalika.

 

Krg The Don alisema kuwa yeye ndiye mmiliki wa Nairobi na hakuna mtu ambaye anaweza kufanya tukio kubwa kama hilo bila kumjulisha.

 

Krg The Don aliendelea na kudai kuwa harusi ya Akothee ni ghushi, na lazima arudie harusi hiyo, la sivyo ataharibu vyeti vyao vya ndoa.

 

“Iko Msichana mjaluo amefanya harusi hii town. Ameoa mzungu, mimi ndio mwenye town, na hio harusi ya Akothee ni fake, lazima angenijulisha juu mimi ndio mwenye town. Akothee lazima arudie hio harusi amaharibu ni makaratasi yao.”

 

Akothee alifunga pingu za maisha na mumewe, Dennis Schweizer, kwa jina la utani Omosh, jana kwenye harusi kuu iliyofanyika Windsor Golf Hotel jijini Nairobi.

 

Tukio hilo lilijaa fahari huku wageni wakiwasili kwa mtindo wa sherehe ya mwaliko pekee.

 

Watu mashuhuri na wanasiasa wa Kenya walipamba sherehe hiyo huku mama huyo wa watoto watano akisema “YES I DO ,” kwa upendo wa maisha yake.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!