Pope Francis Aondoka Hospitalini Baada Ya Kutibiwa

Papa Francis ameondoka hospitalini mjini Roma ambako ametumia siku chache zilizopita akitibiwa ugonjwa wa kupumua.
Papa francis mwenye umri wa miaka 86 alipelekwa katika hospitali ya Gemelli siku ya Jumatano na alipewa dawa za kutibu ugonjwa wa mkamba unaoambukiza.
Papa – ambaye alipokuwa kijana aliugua nimonia kali na sehemu ya pafu kuondolewa – amekuwa na msuruo hivi majuzi wa masuala ya matibabu.
Mara nyingi ameonekana akiwa na fimbo na wakati mwingine hutumia kiti cha magurudumu kutokana na maumivu katika goti lake la kulia.
Mwaka jana, alighairi safari ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Sudan Kusini baada ya madaktari kusema kwamba anaweza pia kukosa safari ya baadaye ya Canada isipokuwa alikubali kuwa na siku 20 zaidi za matibabu na kupumzika kwa goti lake.
Papa Francis pia anaugua (diverticulitis), hali ya kawaida ambayo inaweza kusababisha kuvimba au maambukizi ya koloni… Mnamo 2021, alifanyiwa upasuaji wa kuondoa sehemu ya utumbo wake.
Papa anatarajiwa kushiriki katika ibada ya Jumapili ya Palm katika uwanja wa St Peter’s Square.