Kina mama hao ambao wanaonekana katika hali ya kutia huruma, waliinua mikono yao juu na kupiga magoti wakiwaomba polisi kusitisha kuwatupia vijana vitoza machozi, kwani kufanya hivyo ni kama kuwachochea kuzidi kujibu kwa kuwatupia mawe pia, na hivyo kuhatarisha hali nzima ya maandamano hayo ambapo baadhi wanaumia kwa kujeruhiwa, na pia vitoa machozi hivyo vinawaathiri kina mama hao na watoto wadogo katika nyumba zao.
Hata hivyo, dua ya akina mama hao yaliangulia patupu baada ya vijana kujitokeza na kuanza kurusha mawe na kusurutisha polisi kuwatimua kwa kurusha vitoa machozi na wakatawanyika bila ya maombi yao kukubaliwa.
Hayo yanafuatia kuitishwa kwa maandamano na kiongozi wa Azimio Raila Odinga ambapo ameongoza wafuasi wake kuipinga serikali Alhamisi maeneo kadhaa jijini Nairobi. Katika maandamano hayo, kumeshuhudiwa vurugu, wizi wa mali ya watu, mauaji na uhalifu wa aina tofauti tofauti nchini.