Home » Rais Ruto Aaomba Mataifa Ya Afrika, Pasifik Kuimarisha Uhusiano Na Umoja Wa Ulaya

Rais Ruto Aaomba Mataifa Ya Afrika, Pasifik Kuimarisha Uhusiano Na Umoja Wa Ulaya

Rais William Ruto amelitaka Shirika la Mataifa ya Afrika, Karibea na Pasifiki (OACPS) kuboresha uhusiano na Umoja wa Ulaya ili kufungua fursa za biashara na uwekezaji kwa wanachama wake.

 

Rais amesema kucheleweshwa kwa kusainiwa kwa mikataba muhimu, kama vile Mkataba wa Ushirikiano wa Baada ya Cotonou (Samoa), kumezuia fursa nyingi kwa nchi wanachama na kulitaka shirika hilo kushirikisha EU ili kuanzisha muundo wa faida.

 

Hayo ameyazungumza wakati wa kikao na ofisi ya kamati ya mabalozi wa OACPS ikiongozwa na Katibu Mkuu Georges Rebelo Pinto Chikoti.
Rais Ruto pia ameitaka OACPS kuunganisha nchi wanachama ili kuimarisha nafasi ya mazungumzo ya kanda.

 

Ameibua wasiwasi juu ya athari za kijamii na kiuchumi za sheria ya Mpango wa Kijani wa Ulaya kwa nchi zinazouza nje.

 

Rais amesema sheria hiyo itasababisha kuongezeka kwa gharama za kufuata sheria na kuzorota kwa jumla kwa biashara na kusababisha kuongezeka kwa umaskini.

 

Balozi wa Jamhuri ya Mauritius na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa OACPS, S. Gunessee, Balozi wa Jamhuri ya Cameroon na Mkuu wa Kamati ya Mabalozi, Daniel Evina Abe’e, Makatibu wa Baraza la Mawaziri Alfred Mutua (Mambo ya Nje na Diaspora) , Susan Nakhumicha (Afya), Njuguna Ndungu (Fedha), Soipan Tuya (Mazingira) na Kipchumba Murkomen (Barabara na Uchukuzi) pia walikuwepo.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!