Home » Kylian Mbappe Ateuliwa Nahodha Wa Timu Ya Taifa Ya Ufaransa

Kylian Mbappe Ateuliwa Nahodha Wa Timu Ya Taifa Ya Ufaransa

Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 24 amechaguliwa na Didier Deschamps kuwa nahodha wa timu ya taifa ya france, Les Bleus , kufuatia kustaafu mechi ya kimataifa kwa mlinda lango Hugo Lloris.

 

 

Wengi walikuwa wanampigia upato Antoine Griezmann kuchukuwa nafasi hiyo lakini Deschampas akampendekeza Mbappe, mzaliwa wa Bondy.

 

Mnamo Februari, shirika la Get French Football News iliripoti kwamba Mbappé alikuwa kwenye mstari wa kutwaa unahodha kama mgombea anayeongoza akiwa na umri wa miaka 24 tu. Hii ilifuatia  wimbi la kustaafu kwa wachezaji wazoefu wa ufaransa akiwemo Steve Mandanda  mwenye umri wa miaka 37, Karim Benzema ( 34), na Raphaël Varane (29) ambaye alikuwa naibu nahodha wa Les Bleus.

 

 

Kufuatia uamuzi huo, Hugo Lloris alimuunga mkono Mbappé kumrithi kama nahodha siku ya Jumapili alipokuwa akizungumza na Téléfoot. Kipa huyo wa Tottenham Hotspur alitangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa kufuatia kushindwa kwa Ufaransa katika fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina mwezi Desemba.

 

 

Didier Deschamps leo alisema kuwa atafanya mazungumzo na Mbappé kuhusu unahodha wa Ufaransa, huku maamuzi yakitarajiwa kutangazwa rasmi siku ya Alhamisi.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!