Home » Aliyekuwa Miss Universe Kenya Rachel Mbuki Atengana Na Mumewe

Aliyekuwa Miss Universe Kenya Rachel Mbuki Atengana Na Mumewe

Aliyekuwa Miss Universe Kenya Rachel Mbuki ametangaza kutengana na mumewe, Litvishkova.

 

Mwanamitindo huyo mkongwe, ambaye pia ni mwigizaji na mtangazaji wa TV, alitoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Instagram akieleza masikitiko yake juu ya uamuzi huo na kuongeza kuwa ataomba talaka hivi karibuni.

 

“Ni kwa masikitiko makubwa kwamba ninatangaza kwamba mimi na mume wangu tumefikia uamuzi mgumu wa kuvunja ndoa yetu. Kwa sasa tumetengana, na ninawasilisha kesi ya talaka,” Mbuki aliandika.

 

“Najua hii inakuja kama mshtuko kwenu nyote kwa sababu mliwekeza sana kwetu pia, lakini natumai tunaweza kuendelea kutegemea upendo na msaada wenu tunapovuka hatua hii mpya,” aliandika.

 

Mbuki pia aliwashukuru marafiki zake wa karibu na familia kwa usaidizi wao na alikiri kwamba tangazo hilo liliwashtua.

 

Talaka hiyo ya kushangaza inajiri miezi michache tu baada ya Mbuki kuwa ‘surprised’ na Ksh.10 milioni za Porsche Cayenne na mumewe.

 

“Mume wangu amefanya jambo leo. Alini-surprise na Porsche Cayenne la Platinum la 2023! Asante kwa mume bora zaidi. Ninakupenda sana!!!!” aliandika.

About The Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

error: Content is protected !!