Southampton Yapiga Breki Makali Ya Tottenham Ligi Kuu EPL

Hatima ya Tottenham ya kumaliza katika nafasi nne bora kwenye Ligi ya Premia ilitibuka baada Southampton kulazimish sare ya 3-3 siku ya Jumamosi, huku Leeds wakiongeza matumaini yao ya kunusurika kwa ushindi wa 4-2 dhidi ya Wolves.
Spurs walionekana kuwa tayari kuipiku Manchester United hadi nafasi ya tatu walipoongoza kuwa mbele magoli 3-1 zikiwa zimesalia dakika 13 pekee mchezo kumaliza
Lakini bao la kwanza la Theo Walcott katika takriban miaka miwili na mkwaju wa penalti wa dakika za majeruhi wa James Ward-Prowse uliipa Southampton muhimu
Hata hivyo droo hiyo inaiwacha southamptom katika nafasi mbaya zaidi kwani bado wanaburura mkia na kuwa hatarini kushushwa ngazi.
Tottenham wanashikilia nafasi 4 kwa sasa na alama 49, alama moja nyuma ya machester unite wanaoshikilia nafasi ya tatu.